Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madiwani wengine Chadema wahamia CCM

Madiwani wengine Chadema wahamia CCM

Fri, 13 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Madiwani wawili wa Chadema katika Jiji la Arusha wamejiuzulu na kuhamia CCM kwa maelezo kuwa wanataka kumuunga mkono Rais wa Tanzania, John Magufuli.

Madiwani hao ni Isaya Doita (Ngarenaro) na Damuni Melamari wa Sakina.

Amejiuzulu juzi jioni Jumatano Machi 11, 2020 , taarifa zao zilianza kusambaa jana katika mitandao ya kijamii.

Akizungumza leo Ijumaa Machi 13, 2020,  Doita amesema amejiuzulu ili kuunga mkono kazi inayofanywa na kiongozi mkuu huyo wa nchi pamoja na mkuu wa Wilaya ya Arusha, ,Gabriel Daqaro na mkurugenzi wa Jiji hilo, Dk Maulid Madeni.

Dk Madeni amethibitisha kupokea barua za kujiuzulu kwa madiwani hao.

Mwenyekiti wa chadema wilaya ya Arusha, Ephata Nanyaro amesema, “nimepokea taarifa zao tulijua kitambo wataondoka na bora wameondoka.”

Pia Soma

Advertisement

Aliyekuwa Meya wa  Jiji la Arusha, Calist Lazaro ambaye hivi karibuni alihamia CCM akitoka Chadema, amesema madiwani  hao wameondoka katika chama hicho kwa ajili ya kuachana na siasa zisizo na tisa.

Kuhama wa madiwani hayo kunakifanya Chadema kubaki na madiwani 13 huku CCM wakiwa tisa katika Jiji la Arusha, baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, Chadema walikuwa na madiwani 33 na CCM diwani mmoja.

Chanzo: mwananchi.co.tz