Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madiwani wawili Chadema wajiuzulu, waomba kuhamia CCM

24993 Diwani+pic TanzaniaWeb

Thu, 1 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Babati. Wimbi la madiwani wa Chadema mkoani Manyara kujiuzulu na kujiunga na CCM limeendelea kushika kasi baada ya madiwani wengine wawili kufuata nyayo za wenzao.

Madiwani hao ni Eluthery Burra (Dareda) na Yakobo Nini (Makame).

Akizungumza na Mwananchi leo Alhamisi Novemba Mosi, 2018 mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Babati, Hamis Malinga amesema amepokea barua za kujiuzulu za wawili hao.

Malinga amesema Burra ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) jimbo la Babati katika barua yake aliandika kuwa anataka kujiunga na CCM.

“Amejiuzulu nafasi yake kwa kuandika barua na kuomba kujiunga na CCM kwa lengo la kumuunga mkono Rais John Magufuli na mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti," amesema Malinga.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Kiteto, Tamim Kambona amesema Nini ameandika barua ya kujiuzulu nafasi hiyo na kuomba kujiunga na CCM.

"Tupo katika mchakato wa kuandika barua kwenye Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ili uchaguzi mdogo ufanyike baada ya diwani huyo kujiuzulu nafasi hiyo," amesema Kambona.

 

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz