Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madiwani wawili Chadema wahamia CCM

20108 Pic+chadema TanzaniaWeb

Mon, 1 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Serengeti. Ngome ya Chadema wilayani hapa inazidi kuporomoka kufuatia madiwani wawili akiwemo makamu mwenyekiti kubwaga manyanga.

Ndani ya siku tatu toka amejivua nyadhifa zote ikiwemo ubunge, Marwa Ryoba na kuhamia CCM, madiwani watatu wameshajitoa hali ambayo inaonyesha wazi chama hicho kiko hatarini kupoteza halmashauri.

Waliojivua nyadhifa na kuthibitishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo Juma Hamsini ni Pasto Maiso kata ya Ring'wani ambaye alikuwa makamu mwenyekiti wa halmashauri kwa vipindi viwili.

Mwingine ni George Mahemba kata ya Magange ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Masinki kupitia Chadema.

Katika barua zao za jana Septemba 29, 2018, wamedai sababu za kujivua uanachama wa Chadema ni kuunga juhudi za Rais John Magufuli za maendeleo na kutetea wanyonge.

Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Juma Porini kwa mshangao amesema ameongea na Maiso na kumthibitishia hajapeleka barua, "Kama amekataa wakati amepeleka hilo liko juu ya uwezo wangu."

Katika uchaguzi wa mwaka 2015 Chadema ilishinda kata 18 na  CCM 12, ambapo walipata viti maalum saba na mbunge mmoja na kufikisha idadi ya wajumbe 26, dhidi ya 16 wa CCM.

Mwanzoni mwa mwaka huu madiwani wawili wa kata za Ikoma na Manchira walijivua uanachama wa Chadema na katika uchaguzi mdogo CCM ilipita bila kupingwa na kufikisha kata 14 kati ya 16 za Chadema.

Kujitoa kwa madiwani wawili na mbunge, Chadema inapoteza wajumbe watatu na kama CCM itashinda nafasi hizo itakuwa na wajumbe 21 dhidi ya 20 wa Chadema hali inayotishia utawala wa chama hicho kuanguka.

Chanzo: mwananchi.co.tz