Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madiwani watatu wa Chadema Arusha wahamia CCM

92887 Pic+madiwani Madiwani watatu wa Chadema Arusha wahamia CCM

Fri, 24 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Madiwani watatu wa Chadema katika Jiji la Arusha wamejiuzulu na kuhamia CCM kwa maelezo kuwa wanaunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais wa Tanzania, John Magufuli.

Madiwani hao ambao taarifa za kujiuzulu zilianza kusambaa usiku wa kuamkia leo Ijumaa Januari 24, 2020  ni Welance Kinabo (Themi), Zakaria Mollel (Oloirien) na James Lyatuu (Unga Limited).

Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Dk Maulid Madeni amethibitisha kupokea barua za madiwani hao kujiuzulu, “nimepokea barua zao nitatoa taarifa baadaye.”

Katika uchaguzi mkuu mwaka 2015,  diwani wa CCM alikuwa mmoja na wa Chadema 25 lakini kutokana na madiwani kadhaa kujiunga na CCM hadi sasa chama hicho tawala kina wanane na Chadema 15.

Hivi karibuni aliyekuwa Meya Jiji la Arusha, Kalist Lazaro alijiuzulu na kujiunga na CCM.

Endelea kufuatia Mwananchi kwa taarifa zaidi

Pia Soma

Advertisement

Chanzo: mwananchi.co.tz