Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madiwani waichangia kuinusuru shule kongwe

D65c35903a16bb44843dfa9e80a6eb7d Madiwani waichangia kuinusuru shule kongwe

Mon, 22 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

MADIWANI wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma wamechangia mifuko 100 ya saruji yenye thamani ya Sh milioni 2.7 kwa ajili ya kukarabati Shule ya Msingi ya Hombolo- Makulu iliyopo jijini Dodoma iliyojengwa kabla ya kupata uhuru Desemba 9, 1961.

Akipokea mifuko hiyo kwa niaba ya Kamati ya Siasa ya Wilaya hiyo, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Dodoma Mjini, Salingo Risasi alishukuru madiwani kwa msaada huo ulilenga kurejesha heshima ya shule hiyo.

Akizungumza na waandishi jijini hapa mwishoni mwa wiki, Risasi alisema, uchakavu wa majengo wa shule hiyo kongwe ulionwa wakati ziara iliyofanywa na kamati yake kukagua masuala ya elimu, afya na miundombinu ya barabara.

'Kamati ya siasa baada ya kutembelea shuleni hapo walibaini uchakavu wa majengo ya shule na ndipo madiwani wakaazimia kuichangia shule hiyo iliyojengwa mwaka 1952 wakati wa ukoloni," alisema.

Naye Katibu wa Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Edward Maboje alisema, mchango huo ni sehemu ya juhudi zao katika kutambua umuhimu wa elimu ambapo wameweza kukubaliana kwa pamoja ili kufanya ukarabati katika shule hiyo kongwe ambayo hivi sasa imechakaa.

Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Dodoma Josephat Maganga akipokea mifuko hiyo ya saruji kwa niaba ya serikali alisema, mifuko hiyo ataiwasilisha Hombolo-Makulu ili kufanya ukarabati wa shule hiyo.

Chanzo: habarileo.co.tz