Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madiwani wa Chadema Mbeya waendelea kukimbilia CCM, Chadema kuikosa halmashauri

98695 Pic+mawiwani Madiwani wa Chadema Mbeya waendelea kukimbilia CCM, Chadema kuikosa halmashauri

Wed, 11 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mbeya. Ngome ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jijini Mbeya imeendelea kutetereka baada ya madiwani watatu kuhamia CCM. Kuhama kwa madiwani hao kunafanya idadi ya waliohama kutoka Chadema kwenda CCM kufikia 14 ambapo Januari 26 mwaka huu madiwani 11 wakiongozwa na aliyekuwa mstahiki meya Mchungaji David Mwashilindi walihamia CCM. Kutokana na kuhama kwa madiwani hao hivi sasa CCM inakuwa na madiwani 17 huku Chadema ikiwa na madiwani 16 hivyo kuifanya Chadema kuipoteza Halmashauri ya Jiji la Mbeya. Katibu mwenezi wa CCM mkoani Mbeya, Bashiru Madodi amesema kuwa hamahama hiyo inafanya CCM kuwa na madiwani 17 huku Chadema wakiporwa halmashauri kwa kuwa na madiwani 16.

Chanzo: mwananchi.co.tz