Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madiwani chagueni viongozi wanaojitambua

0d43d1699d9c3d037206c2565912d71d Madiwani chagueni viongozi wanaojitambua

Mon, 23 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

HIVI KARIBUNI Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ilikuwa na kazi kubwa ya kuchekecha na kuja na majina ya wagombea wa nafasi za mameya wa majiji, Manispaa, Wenyeviti wa Halmashauri za wilaya na Halmashauri za Miji.

Imeelezwa kuwa chekeche hilo lilifanyakazi ngumu sana ya kuteua na kuthibitisha wanaogombea nafasi hizo kutokana na kuwapo kwa majina mengi.

Ingawa kuna maeneo yamerudi majina mawili au jina moja au mawili kulingana na matakwa ya Kamati Kuu, kwa kazi iliyofanyika ya uteuzi na uthibitishaji, salamu zipo wazi kuhusiana aina ya uongozi unaotakiwa katika ngazi hizo zinazogusa tawala za mikoa na serikali za mitaa moja kwa moja.

Pamoja na ukweli kuwa zipo baadhi ya Halmashauri za miji na wilaya ambazo zinatakiwa kurudia uchaguzi mara moja kulingana na matakwa ya Chama Cha Mapinduzi ili kufanya kazi hiyo vizuri zaidi na kwa tija, tunapenda kuwakumbusha wahusika kwamba nafasi hizo ni kaa la moto kutokana na mahitaji yake kwa sasa.

Wakati kamati Kuu ya CCM inaangalia viongozi watakaokwenda na kasi ya Rais Magufuli ili wasiwe na shaka nao, wawe na maadili na wachapa kazi; sisi tunasema kwamba ukuaji wa uchumi ndani ya jamii unahitaji viongozi wanaojiongeza na madiwani wasifanye makosa.

Hivyo shime madiwani wakati wa kupiga kura ni lazima kumhoji namna ambavyo mwenyekiti au meya anavyoweza kuongoza Baraza hilo madiwani kufikisha Halmashauri husika katika uchumi wa viwanda wakifungua zaidi soko la wakulima, wavuvi na wafugaji.

Tunaamini kwamba kwa sasa hatuhitajik mzaha kwani viongozi watakaoshindwa kuwezesha kero za wananchi kutatuka hatakuwa anatufaa kwa maendeleo yetu.

Tunachotaka kusema madiwani wawe waangalifu na viongozi wao na kamati zao ili katika kila halmashauri wakulima na wafugaji ambao ndio wengi waweze kuwa na uhakika wa soko la mazao yao kwa kufanya kila juhudi halmashauri kuwa na kiwanda kinachohusiana na mali ghafi zilizopo kwenye eneo hilo.

Kwa kuwa katika Halmashauri ndiko fedha zinakoenda, kitendo chochote cha kuwa na kiongozi anayengoja kutafuniwa itakuwa ni balaa tupu kwa ustawi wa wananchi.

Hakika ili tuvuke salama katika safari yetu nzito ya kuwezesha maendeleo katika maeneo yote ili kusaidia kuimarisha uchumi wa kati, madiwani ni lazima kuwa na uhakika na viongozi wanaowachagua kwamba watawaongoza katika maono ya halmashauri yao kuwa na kiwanda cha kuchakata mazao waliyokuwa mathalani maeneo yanayolima mahindi na soya kwa wingi.

Tunaamini hapa kwamba kama kila halmashauri itawezesha watu wake kuwa na kiwanda cha kuongezea thamani bidhaa za mkulima zitasaidia mwishoni mwa safari kuwa na viwanda vingi vinavyojali kuinua maisha ya mkulima kwa kumpa soko.

Wakati umefika kwa mabaraza hayo kutambua kwamba wananchi wanyonge wanangoja kupewa nafasi ya kuuza bidhaa zao lakini fursa hiyo ni kuwa na soko, soko ambalo linahusiana na uongezeji wa thamani unaoweza kufanyika tu katika kiwanda iwe kidogo au cha kati.

Pamoja na kutoa heri kwa mabaraza yote kuchagua viongozi wanaojielewa na kuelewa, tunapenda kueleza kwamba kila mmoja akifanya uchaguzi wenye neema atafarijika kuona kwamba mazao ya wakulima yanaongezewa thamani na kuleta utajiri kwake.

Ndio kusema tunawaomba madiwani kuangalia maslahi mapana ya wananchi wao katika ujenzi wa taifa na halmashauri husika na kujua ukweli kuwa kupanga ni kuchagua na hakika wanachagua maendeleo ya kasi kwa jamii yao.

Chanzo: habarileo.co.tz