Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madiwani Chadema, NCCR wahamia CCM

10409 Chadema+pic TanzaniaWeb

Mon, 6 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Bukoba. Madiwani wawili wa Chadema na NCCR-Mageuzi  manispaa ya Bukoba wamejiuzulu uanachama na kujiunga na CCM, Akiwemo meya wa zamani wa manispaa hiyo, Dk Anatory Aman.

Dk Aman  aliyekuwa diwani wa Kagondo Agosti 20, 2015 alihama CCM na kujiunga na NCCR-Mageuzi na kuwania udiwani katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, 2015.

Mbali na Dk Aman, mwingine ni aliyekuwa diwani wa Hamugembe (Chadema), Muhaji Kachwamba. Wote wameshakabidhi  barua za kujivua nyadhifa zao katika ofisi za CCM Mkoa wa Kagera tukio lililoshuhudiwa na viongozi mbalimbali.

Akitaja sababu za kurejea CCM, Dk Aman amesema ameridhishwa na utendaji kazi wa Rais John Magufuli.

Amesema CCM ni sehemu sahihi ambayo anaweza kumsaidia Rais Magufuli kutekeleza ilani ya chama hicho tawala, kubainisha kuwa ameondoka NCCR na waliokuwa wakimuunga mkono.

Mwenyekiti wa CCM manispaa ya Bukoba, Ioas Muganyizi amesema milango bado ipo wazi kwa wanachama wengine wanaotaka kujiunga na chama hicho.

Chanzo: mwananchi.co.tz