Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mabunge ya Tanzania, Morocco kushirikana

Tulia Morocco Mabunge (600 X 342) Mabunge ya Tanzania, Morocco kushirikana

Tue, 19 Sep 2023 Chanzo: mwanachidigital

Spika wa Bunge la Dk. Tulia Ackson, amekutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Spika wa Bunge la Morocco Rachid Talbi El Alami katika ofisi za Bunge hilo zilizopo Jijini Rabat nchini Morocco leo tarehe 18 Septemba, 2023.

Pamoja na mambo mengine, Viongozi hao wamejadili kuhusu namna bora ya kuimarisha uhusiano na ushirikiano baina ya Mabunge ya nchi hizo mbili hususani katika sekta ya kilimo, viwanda na biashara.

Aidha, Dk.Tulia ametumia nafasi hiyo kutoa pole kwa Serikali ya Morocco kwa vifo vya watu zaidi ya 3000 na madhara yaliyosababishwa na tetemeko la ardhi lililoikumba nchi hiyo mapema mwezi huu.

Pia amepongeza juhudi zilinazofanywa na Mfalme Mohammed wa VI wa Morocco katika kukabiliana na maafa pamoja na changamoto zilizotokana na tetemeko hilo.

Chanzo: mwanachidigital