Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mabilionea wote ni zao la CCM - Dkt Nchemba

NNNNNNNNN Mabilionea wote ni zao la CCM - Dkt Nchemba

Fri, 5 Nov 2021 Chanzo: eatv.tv

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema kuwa serikali imeweka mpango mkakati wa kuwainua wafanyabishara wadogo wadogo ili waweze kufikia hatua za kuwa mabilionea na kuongeza idadi ya mabilionea nchini.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Novemba 4, 2021, Bungeni jijini Dodoma, wakati akijibu swali la Mbunge Halima Mdee kuhusu suala la wamachinga.

"Serikali ya CCM inawajali sana wafanyabiashara wadogo, na uthibitisho mmoja ni kwamba mabilionea wote walioko katika nchi hii ni zao la Chama cha Mapinduzi kwa sababu hakuna chama kingine kimewahi kuongoza," amejibu Waziri Nchemba   

Chanzo: eatv.tv