Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maalim Seif kuzikwa leo Pemba

912bda852dd50123210ac3ee54caa765 Maalim Seif kuzikwa leo Pemba

Thu, 18 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

S ERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar(SMZ) imetangaza kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais , Maalim Seif Shariff Hamad atazikwa leo kijijini kwao Daya Mtambwe kisiwani Pemba.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Uratibu na Baraza la Wawakilishi, Dk Khalid Salum Mohamed alisema mwili wa marehemu utaswaliwa leo majira ya saa 3:00 asubuhi katika Msikiti wa Maamur uliopo Upanga jijini Dar es Salaam kisha kusafirishwa kwenda Unguja.

“Mwili wa marehemu ukifika Unguja utaswaliwa katika Msikiti wa Hospitali ya Mnazimmoja na wananchi kupata nafasi ya kutoa salamu za mwisho kabla ya kusafirishwa kwenda Pemba,”alisema.

Baada ya kuwasili kisiwani Pemba, mwili wa Maalim Seif utaswaliwa katika Uwanja wa Gombani, ambapo wananchi watapata fursa ya kumuaga mpendwa wao na maziko yatafanyika mchana.

Chanzo: habarileo.co.tz