Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maalim Seif awavuruga CUF, Chadema Lindi

542438ca5a2d2890b3aa9f45d11e62fe Maalim Seif awavuruga CUF, Chadema Lindi

Sat, 25 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MWENYEKITI wa Chama Cha ACT – Wazalendo, Maalim Seif Shariff Hamad jana alipokea wanachama wanane kutoka Chama Cha Wananchi (CUF) mjini Lindi. Pia Maalim Seif alifungua matawi katika mitaa ya Tulieni, Chikonji, Jangwani na alipokea wanachama wapya 55.

Kiongozi huyo wa ACTWazalendo aliwataka wanachama na wapenzi waliojiunga na chama hicho kuwa makini kutetea haki zao. Alitaka ziwepo kamati za uongozi ndani ya kata zenye wajumbe 15, zifanye kampeni kwenye mitaa na kuhakiki wanachama.

“Sisi kwetu Pemba tulishajua wazi kura za Rais, wabunge na masheha kabla ya uchaguzi, kwani tunahakiki mara kwa mara kuanzia ngazi ya kata, Sheha na kuzilinda kura,” alisema Maalimu Seif jana.

Maalim Seif alipongeza wanachama Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa kutoa haki kwa wanachama waliotoka kambi za upinzani waliojiunga na CCM hivi karibuni kisha kugombea ubunge, kwani wameshindwa vibaya katika kura za maoni.

Mwenyekit wa ACT-Wazalendo Mkoa wa Lindi, Isihaka Mchinjita alisema mkoa wote una wagombea kwenye ubunge na madiwani. Alisema kuwa amegawa kadi 30,000 za chama hicho na bado zinahitajika, kwa kuwa wanachama wengi kutoka CUF na Chadema wanajiunga na chama hicho.

Chanzo: habarileo.co.tz