Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maalim Seif atoa sababu kugombea Mwenyekiti wa ACT- Wazalendo

93760 Maalim+pic Maalim Seif atoa sababu kugombea Mwenyekiti wa ACT- Wazalendo

Fri, 31 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Unguja. Mshauri Mkuu wa Chama cha siasa nchini Tanzania cha ACT- Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad amechukua fomu ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti Taifa wa chama hicho.

Maalim Seif amechukua uamuzi huo baada ya uongozi wa ACT- Wazalendo Januari 27, 2020 kutangaza kuanza mchakato wa uchukuaji na urejeshaji wa fomu kuwania nafasi mbalimbali.

Maalim Seif amechukua fomu hiyo leo Alhamisi Januari 30, 2020 ofisi ndogo ya chama hicho Vuga Mjini Unguja na kukabidhiwa na Kaimu Katibu Mkuu wa ACT- Wazalendo, Doroth Semu.

Baada ya kupewa fomu, Maalim Seif amesema sababu kuu ya kuwania nafasi hiyo inatokana na uwezo wake pamoja na uzoefu alionao wa kisiasa kwa zaidi ya miaka 25 hivi sasa.

Amesema kupitia uzoefu huo ana amini nafasi ya uenyekiti taifa ataweza kuihudumia kwa lengo la kuleta mabadiliko makubwa ndani ya Chama hicho, ambacho hivi sasa kinapanga safu zake za uongozi kwa mujibu wa katiba.

"Iwapo wanachama watanipa ridhaa ya kuwa mwenyekiti, basi nitasimamia nidhamu na uwajibikaji katika chama chetu ili kujenga chama imara na kikuu cha siasa Tanzania na kuleta mabadiliko wayatakayo wananchi," amesema Maalim Seif aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF)

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement
Kwa upande wake, Dorothy amesema kwa mujibu wa katiba ya chama hicho, nafasi hizo zipo wazi kwa kila anayetaka kugombea ambaye ametimiza taratibu za kikatiba ya Chama hicho.

Uchukuaji wa fomu ulianza Januari 27,2020 mpaka Februari 26, 2020.

Machi 7, 2020 utafanyika uchaguzi ngome ya wazee; Machi 8, 2020 ni uchaguzi ngome ya vijana, Machi 9, 2020 ni uchaguzi ngome ya wanawake na Machi 14, 2020 itakuwa ni uchaguzi wa chama.

Nafasi zitakazogombewa ngazi ya Taifa ni kiongozi wa chama, naibu kiongozi, mwenyekiti wa Taifa, makamu mwenyekiti Taifa - Tanzania Bara na Zanzibar, katibu mkuu, wajumbe wa halmashauri kuu (nafasi 15) na wajumbe wa kamati kuu (nafasi nane) uchaguzi wa viongozi wakuu utafanyika Machi 14, 2020 ukitanguliwa na chaguzi nyingine za ngome ya wazee, ngome ya vijana na ngome ya wanawake.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz