Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maalim Seif atangaza maamuzi haya

SEI Maalim Seif atangaza maamuzi haya

Sat, 20 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo Taifa, Maalim Seif Sharif Hamad, amesema kuwa mpaka sasa tayari amekwishafanya maamuzi ya dhati na hivi karibuni atayatangaza na hivyo wananchi wajiandae.

Maalim Seif ametoa kauli hiyo leo Juni 20, 2020, jijini Dar es Salaam, katika mkutano wa chama hicho, ambapo licha ya kusema hivyo hakueleza ni maamuzi gani ambayo amepanga kuyachukua.

"Nimeshafanya maamuzi ambayo nitayatangaza rasmi Juni 28 tukijaaliwa, hivyo jitayarisheni mtayasikia maamuzi yangu ni yapi, na maamuzi haya mtayapenda ninyi nyote" amesema Maalim Seif.

Aidha Maalim Seif akatoa msisitizo suala la Tume huru ya Uchaguzi tanzania, "Mimi namsikia sana Rais Magufuli, juzi Bungeni katuambia kutakuwa na uchaguzi huru na wa haki, lakini ni maneno tu, lakini utapataje Uchaguzi huru na haki, ili hali Tume ya Uchaguzi ni hii hii?".

Chanzo: www.tanzaniaweb.live