Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maajabu Mwanamke, Binti wanavyo iba, kuua watoto

9304b709dc844e1d5d792e9afc9807eb.png Maajabu Mwanamke, Binti wanavyo iba, kuua watoto

Wed, 16 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamke mmoja mkazi wa Geita, Juliet Makoye (43) amepandishwa kizimbani pamoja na binti wa miaka 15 kwa tuhuma za wizi wa mtoto wa miaka 3 na miezi 6 katika mtaa wa Nyakato Mlimani Manispaa ya Musoma mkoani Mara.

Wakili wa Serikali, Monica Hokololo ameiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi Musoma kuwa tukio hilo lilifanyika Februari 10 mwaka huu likimhusisha binti aliyetaka kumuiba mtoto kinyume na Kifungu cha 169 (1)(a) cha Kanuni za Adhabu Na.16 na mapitio yake ya Mwaka 2019.

Katika Kesi hiyo ya Jinai Na.48 ya Mwaka 2022 Wakili Hokololo aliieleza mahakama kuwa, mshtakiwa alimkuta mtoto akiwa amekaa peke yake na kumchukua kisha akamlisha dagaa waliokuwa na dawa kumfanya apoteze uwezo wake wa kuongea. Vilevile alizisuka upya nywele zake na kumbadilisha nguo kabla ya kuita ungo ili aondoke naye, hata hivyo haikuwezekana.

Imedaiwa mahakami hapo kuwa, lengo ilikuwa kumpeleka mtoto huyo Geita kwa njia ya ungo. Wakili alisema wakati wa upelelezi, binti huyo alidai baada ya juhudi za kupata usafiri kushindikana alianza kuzurura hovyo akiwa amembeba mtoto na alipo hojiwa alidai ametoka Geita yeye na mdogo wake na walikuwa wakimtafuta mama yao bila mafanikio.

Binti pamoja na mtoto walipelekwa kwa Mtendaji wa Mtaa wa Kigera ambaye aliwapeleka Kituo cha Kati cha Polisi. Aliendelea kusema kuwa Polisi iliamua kuomba hifadhi katika kituo cha kulelea watoto cha Jipe Moyo mjini Musoma baada ya maelezo ya awali kuonesha watoto hao wamepotea.

Siku moja baada ya kupotea, Wazazi wa mtoto aliyepotea walitoa taarifa polisi, ambapo iliwarejesha tena binti na mtoto kituoni kubaini ikiwa wanauhusiano na taarifa mpya ya wazazi wanaotafuta mtoto wao. Hokololo aliiambia mahakama kuwa, baada ya wazazi kubainisha kuwa mtoto ni wao na binti hawamfahamu ndipo ilipoanza uchunguzi wa kina kuhusu tukio hilo.

Kwa mujibu wa Hokololo, binti huyo amekua akishirikiana na Juliet kuiba watoto wenye umri kati ya miaka miwili na mitano na ikiwa angefanikisha wizi huo idadi ya watoto alioiba ingefikia watano.

Imedaiwa mahakamani hapo kuwa baada ya kuiba mtoto wa jinsia yoyote, Binti huyo na Juliet humchinja, na baadhi ya viongo vya marehemu huuzwa kwa baadhi ya wachimbaji wadogo wa madini mgodini. Alisema, washtakiwa hao hunywa damu za marehemu, na sehemu za mwili huchomwa ama kupikwa na kula ama kuuza katika mgahawa wa Juliet. Wakili Hokololo aliiambia mahakama kuwa “uchunguzi umekamilika.”

Polisi Mkoani Mara ilishirikiana na Polisi Mkoa wa Geita kumkamata Juliet katika Mgahawa kama walivyoelekezwa na binti huyo.

Wawili hao wamekana mashtaka na wamerejeshwa rumande baada ya kushindwa kukidhi masharti ya dhamana ambayo ni kuwa na wadhamini wawili na kila mdhamini kuweka dhamana ya Sh milioni 2 kila mmoja.

Kesi hiyo imeahirishwa na itasomwa tena Machi 28 mwaka huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live