Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maagizo ya Katibu Mkuu CCM kwa Wizara kuhusu matumizi ya fedha za IMF

CHONGOLO12.jpeg Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo

Mon, 18 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo ameziagiza wizara zote zilizopokea mgao wa fedha za mkopo kutoka Shirika la Fedha Duniani (IMF) kutoa mchanganuo wa matumizi kama ilovyofanya Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa mwenyekiti wa chama hicho ambaye ni Rais na Amiri Jeshi Mkuu, Samia Suluhu Hassan katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Chongolo amesema kuchanganua matumizi ya fedha hizo kutaonyesha uwazi kwa wananchi.

"Nampongeza sana Waziri wa Tamisemi (Ummy Mwalimu), amefanya mchanganuo wa matumizi ya fedha zote, wizara nyingine nazo zifanye hivyo," amesema Chongolo.

Chongolo pia amezitaka kamati za siasa za mikoa na wilaya kufatilia matumizi ya fedha zilizopelekwa katika maeneo yao kwani zikipotea watawajibika.

"Kama fedha zitapotea ina maana mtakuwa hamjawajibika," ametahadharisha katibu mkuu huyo wa chama tawala.

Awali, Chongolo alisema CCM imeridhishwa na utendaji wa Rais Samia kwani ndani ya miezi saba ametekeleza vyema ilani na kufanya mambo makubwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live