Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maagizo ya CCM kwa Waziri Aweso juu ya mradi uligharimu Tsh. Bilioni 4.8

MRADI MAJI Mradi wa Maji Mtwara Wasuasua

Wed, 18 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Mtwara , Yusuf Nannila, amemtaka Waziri wa Maji, Jumaa Aweso kufika katika mradi wa maji wa Makonde ambao umesuasua kwa zaidi ya miaka miwili sasa tangu uanzishwe.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea chanzo cha maji cha Mitema kilichopo Kata ya Kitangari, Halmashauri ya Wilaya ya Newala, amesema mradi wa Makonde una matatizo katika utekelezaji na kwamba waziri mwenye dhamana akizembea utekelezaji wake utakuwa ni ndoto.

Nannila amesema maelezo aliyoyapata kutoka kwa wasimamizi wa mradi huo hayaridhishi kwa sababu maelezo yao yanapishana na kile walichojionea kwa macho.

Mradi huo ambao umegharamu kiasi cha shilingi bilioni 4.8 umechukua zaidi ya miaka miwili tangu uanze kutekelezwa huku Nannila akisema serikali imetoa pesa nyingi lakini mradi umechukua siku nyingi kutekelezeka bila sababu za msingi na kusababisha adha kubwa ya maji kwa wananchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live