Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maagizo ya CCM kuhusu zuio la Bodaboda kuingia mjini

2956c72b8d7c5c569126b9ac5995514f Maagizo ya CCM kuhusu zuio la Bodaboda kuingia mjini

Sun, 31 Oct 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kauli ya marufuku ya waendesha bodaboda na bajaji kutofika mjini kwa jiji la Dar es Salaam, si kauli mwafaka na imetolewa bila taratibu za msingi.

Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Shaka Hamidu amesema kuwa maamuzi yatakayotolewa dhidi ya waandesha bodaboda yanapaswa kugusa maslahi ya umma.

“Chama kinaagiza oparesheni hiyo isitishwe mara moja.”amesema Shaka Hamidu.

Aidha Kamishna Msaidizi wa Polisi ambaye ni Mkuu wa Usalama Barabarani, Abdi Issango alisema Ifikapo Septemba 11, 2021 waendesha bodaboda na bajaji marufuku kuingia mjini isipokua bajaji za walemavu.

Chanzo: www.habarileo.co.tz