Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MAMA SAMIA: CCM INA KILA SABABU YA KUCHAGULIWA KWENYE UCHAGUZI HUU

Capture 115.png?fit=774%2C513 MAMA SAMIA: CCM INA KILA SABABU YA KUCHAGULIWA KWENYE UCHAGUZI HUU

Tue, 20 Oct 2020 Chanzo: zanzibar24.co.tz

Mgombea mwenza wa rais wa Jamuhuru ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha mapinduzi Samia Suluhu Hassan amesema ccm ina kila sababu ya kuchaguliwa na watanzania kwenye uchaguzi mkuu wa tarehe ishirini na nane mwezi huu  kwakuwa imetekeleza  ahadi ilizoahidi kwa wananchi  kwenye ilani iliyopita zaidi ya  asilimia tisini na tisa.

Akihutubia mkutano wa kampeni wa kuwaombea kura mgombea urais wa jamuhuri ya muungano wa tanzania Dr John Pombe Magufuli na Dr Hussein Ali Mwinyi anayewania urais wa Zanzibar huko Paje Wilaya ya kusini leo Samia ambaye pia ni makamu wa Rais wa Tanzania ameahidi ccm kuendelea kuwafanyia mambo makubwa watanzania.

Mjumbe huyo wa kamati kuu taifa ya ccm amesema CCM imetekeleza ilani ya uchaguzi  ya mwaka 2015/2020 kwa asilimia 99.9 na maendeleo hayo yaliyofikiwa ni kutokana na usimamizi mzuri wa sera za Serikali zote mbili zilizopo chini ya CCM.

Aidha mama Samia amewaomba wazanzibar wote bila kujali itikadi ya vyama vyao  kumchagua Dr Hussein Ali Mwinyi kwani licha ya kuwa na uzoefu wa kutosha kwa kuitumikia serikali kwa muda mrefu pia ana maono ya mbali juu ya kuukuza uchumi wa Zanzibar.

Kwa upande wake mgombea urais wa Zanzibar kupitia ccm Dr Hussein Ali Mwinyi amewaahidi wananchi wa wilaya kusini kutatua changamoto ambazo hazikukamilika kwenye kipindi cha uongozi wa Dr Shein za maji,elimu,afya na miundo mbinu ya bara bara.

Pia ameahidi kuwalipa fidia wananchi ambao ardhi yao imechukuliwa kwa ajili ya uwekezaji.lakini kwanza ameanza na suala la dawa za kulevya

Nae Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi ,alisema kampeni za kuwanadi wagombea wa Chama Cha mapinduzi na kuinadi ilani ya CCM ya mwaka 2020/2025 kwa wananchi.

Alisema kampeni hizo zimekuwa za kisayansi kwani wagombea wote wamekuwa wakiwafikia wananchi katika makaazi yao kwa kuwaelezea sera na mambo mbalimbali yaliyotekelezwa na CCM nchini.

Chanzo: zanzibar24.co.tz