Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MAGUFULI: Hesabuni kura hadharani

6729683cd3b87ee4f3dcab285c35acd5 MAGUFULI: Hesabuni kura hadharani

Mon, 20 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

Rais Dk John Pombe Magufuli ameshauri watakaosimamia kura za maoni kuhakikisha kila mgombea anapata haki yake tena kwa uwazi.

Ameyasema hayo leo Ikulu ya Chamwino, Dodoma wakati alipokuwa akiwaapisha viongozi mbalimbali wa Serikali ambapo alitaka viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuhakikisha kila mgombea anapata haki yake tena ikiwezekana kura kuhesabiwa hadharani.

Alisema, “Kura za maoni (Ubunge na Uwakilishi) zitaanza leo na kesho ni matumaini yangu viongozi watakaosimamia basi watasimamia kwa uwazi bila mizengwe ili mwenye haki na apate haki yake...

“…ningetamani viongozi wa chama change (CCM), wakimaliza kupiga kura kwenye kura za maoni leo na kesho, wafanye kama tulivyofanya Halmashauri Kuu, kura zihesabiwe hadharani mbele ya Wajumbe, anayepata zero au ngapi ajulikane palepale, uwazi utaendelea kujenga Chama chetu," amesema Rais Magufuli

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amewakaribisha watalii nchi kwani Tanzania ni salama na haina maambukizi ya ugonjwa wa Corona.

“Naona watalii wanazidi kuja, hongereni sana mnaosimamia Utalii, Tanzania tuko salama, Maadui zetu watasema mengi ila tupo salama, hata hapa hatujavaa barakoa, kwani sisi hatuogopi kufa!?, corona ipo mbali kule tuliimaliza, Watali waje tu watakuwa salama,” alihitimisha.

Chanzo: habarileo.co.tz