Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lusinde: Mawaziri jihadharini na Dkt Tulia.....

FINAL LIVINGSTONE.mp4.08 17 20 39.Still001 1140x640 Livingstone Joseph Lusinde, Mbunge wa Mvumi

Tue, 15 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Mvumi kupitia chama cha Mapinduzi CCM, Livingstone Joseph Lusinde amesema uzoefu wa miaka sita ya uongozi kwa Spika mpya wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson utamsaidia kuungoza vyema mhimili huo

Amesema umahiri wa kiongozi huyo katika kusimamia kanuni na taratibu za bunge utasaidia kwa kiasi kikubwa kwa Bunge kulisimamia serikali kikamilifu

“Ninahakika baadhi ya mawaziri wanahitajika kuwa waangalifu katika kuleta taarifa zao bungeni wanaweza wakakutana na kisiki cha kwanza ni Tulia Ackson,”. Amesema Mbunge Lusinde.

Ameongeza kuwa Dkt Tulia ni muumini wa matokeo na maendeleo ya haraka hivyo anategemea kuona akiwabana kisawasawa mawaziri

Lusinde ameyasema hayo kwenye mahojiano maalumu aliyofanya na Dar24 media kuhusu mambo mbalimbali

Chanzo: www.tanzaniaweb.live