Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

‘Lowassa kurejea CCM ni faraja’

45780 Lowassapicc ‘Lowassa kurejea CCM ni faraja’

Mon, 11 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Arusha, Daniel Awakii amesema kurejea ndani ya chama hicho kwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ni faraja kwa chama hicho tawala.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumamosi Machi 9, 2019 wakati wakimpokea Lowassa mkoani humo, Awakii amesema kwa siasa za Tanzania bado Lowassa ni mtu muhimu sana.

"Tumefurahi sana leo kumpokea Lowassa, amerudi CCM na tutashirikiana kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM," amesema.

Katika mapokezi Lowassa amepokelewa pia na wafanyabiashara kadhaa wa madini, viongozi wa CCM mkoa na wilaya ya Monduli pamoja na Godluck Ole Medeye ambaye aliwahi kujiunga na Chadema kabla ya kutimkia Chama cha UDP kisha akarudi CCM.

Soma Zaidi: Fred Lowassa: Tumerejea nyumbani CCM



Chanzo: mwananchi.co.tz