Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lowassa adai deni la Sh60 milioni limempeleka Kalanga CCM

14684 Karannga+pic TanzaniaWeb

Thu, 30 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amesema mgombea ubunge wa CCM Jimbo la Monduli, Julius Kalanga alijiuzulu ubunge baada ya kushindwa kulipa Sh60 milioni alizokopa hivyo alitaka kusaidiwa kuzilipa.

Akizungumza leo Agosti 30 katika mkutano wa kampeni kwenye mji wa Mto wa Mbu, Lowassa amedai baada ya Kalanga kupata fedha alinunua ng'ombe ambao walikufa na sehemu nyingine alilima bila mafanikio huku nyingine akizifanyia starehe.

"Naijua taasisi aliyokopa, akaomba alipiwe deni ndiyo akajiuzulu ili apewe nafasi nyingine,” amesema Lowassa.

Hata hivyo, akizungumza na Mwananchi leo Agosti 30, Kalanga amesema hawezi kulumbana na Lowassa kwa kuwa  anamheshimu.

"Nimesikia anasema nilikopa fedha nimeshindwa kulipa, lakini hii mambo ya kukopa ni mambo binafsi, sitaki kumjibu mzee Lowassa nimewaachia viongozi wa mila Laigwanani wazungumze naye kama kweli ananitendea haki," amesema.

Lowassa amesema sababu alizotoa Kalanga kujiuzulu ikiwamo ile anayosema kuwa Monduli haina maendeleo na haina demokrasia, si za kweli.

"Yeye aseme ameshindwa kuvaa viatu vyangu, aniambie ni wilaya gani imeweza kuleta maendeleo kama Monduli," amesema.

Lowassa amesema kitendo cha Kalanga kujiuzulu   kilikuwa cha ovyo, kimemuudhi na kumkasirisha.

"Kinachoniudhi si kuondoka kwake bali sababu alizotoa kuwa eti Monduli hakuna Maendeleo," amesema.

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz