Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lowassa: Yonas anafaa kuvaa viatu vyangu

15302 Pic+luwasa TanzaniaWeb

Mon, 3 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Monduli. Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, amewataka wakazi wa Monduli, kumchagua mgombea wa ubunge wa Chadema, Yonas Laizer kwani, ndiye anayeweza kuvaa viatu vyake.

Akizungumza jana katika mkutano wa kampeni katika kata ya Makuyuni, Lowassa alisema, Yonas ni kijana msomi ambaye anaweza kutatua kero za wananchi wa Monduli kuliko mgombea wa CCM, Julius Kalanga.

"Ndugu zangu wananchi wa Makuyuni, mchagueni Yonas huyu anaweza kuvaa viatu vyangu ni kijana msomi asiyeyumba kama yule msaliti," alisema Lowassa.

Lowassa katika mkutano huo, pia aliendelea kueleza kusikitishwa na uamuzi wa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Julius Kalanga kuhama Chadema na kujiunga na CCM.

"Tulikuja hapa kumuombea kura Kalanga ametusaliti ametuudhi sana sasa tunzeni heshima ya Monduli kwa kutomchagua tena," alisema.

Kwa upande wake, katibu wa Chadema mkoa wa Arusha, Elisa Mungure amewataka wananchi kuchukizwa na matukio ya baadhi ya wabunge na madiwani kuhama vyama vyao na kujiunga na CCM kwani wanasababisha hasara kwa taifa.

Mungure alisema kutokana na kujiuzulu madiwani katika kata zaidi ya 68, kujiuzuru wabunge watano, zaidi ya Sh30 bilioni ambazo zingetumika kwa shughuli za maendeleo zinatumika katika chaguzi.

"Fedha hizi ambazo serikali ya CCM inazitumia katika chaguzi zingetosha kutatua kero za wananchi masikini," alisema.

Mungure alisema wananchi wa Monduli wanapaswa kuonyesha hasira kwa kutomchagua mgombea wa CCM, Julius Kalanga ambaye alijiuzulu ubunge na kujiunga na CCM.

Chanzo: mwananchi.co.tz