Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lisu abadili mavazi akiwa njiani kuelekea Temeke

Lissuuu Lisu abadili mavazi akiwa njiani kuelekea Temeke

Wed, 25 Jan 2023 Chanzo: Mwananchi

Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu aliyewasili nchini dakika chache zilizopita akitokea Ubelgiji alikokwenda tangu mwaka 2020, amebadilisha mavazi yake akiwa njiani kwenda katika mkutano wa hadhara unaotarajiwa kufanyika mkutano wa hadhara.

Lissu amewasili nchini leo, Januari 25, 2023 alifika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, akiwa amevalia kombati ya kaki ‘gwanda’ ambalo ni vazi linalokitambulisha chama hicho kwa wafuasi wake.

Hata hivyo mwanasiasa huyo machachari akiwa ndani ya gari alionekana amebadili vazi hilo na kuvalia fulana ya mikono mirefu yenye rangi zinazoakisi bendera ya chama hicho. Mara baada ya kubadili vazi hilo, Lissu aliendelea kuwasalimia watu katika kila eneo alilokuwa akipita akiwa juu ya gari.

Chanzo: Mwananchi