Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lissu amjibu Fatma Karume

Lissu Fatma Z Lissu amjibu Fatma Karume

Tue, 30 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Bara, Tundu Lissu, amesema hajafanya makosa kumuita Mzanzibar Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa kuwa ndiyo asili yake. 

Lissu ametoa kauli hiyo jana tarehe 29 Aprili 2024, jijini Dodoma, akizungumza katika mkutano wa hadhara, akimjibu mwanaharakati Fatma Karume, aliyemuita mbaguzi kufuatia hatua yake ya kumtambulisha Rais Samia Mzanzibar wakati anamkosoa.

“Nataka niseme ubaguzi wangu na katiba ya Zanzibar inavyosema, kwenye katiba ya Zanzibar inasema kutakuwa na Mzanzibar haisemi tutakuwa na Mtanzania wa Tanganyika, inasema kutakuwa na Mzanzibar na inasema kila Mzanzibar atafaidi haki na fursa anazostahili Mzanzibar,” amesema Lissu.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X, jana Jumapili, Fatma alihoji iwapo sera ya Chadema ni kutokuwa na Rais wa Tanzania kutoka Zanzibar, baada ya Lissu kusema kuna Rais Samia ni Mzanzibar na sio Mtanganyika.

“Kuna tofauti kubwa baina siasa za hoja na siasa za ubaguzi. Tundu hizi ni siasa za ubaguzi. Ni opportunism na siasa hizi zinaleta manufaa ya mpito tu. Swali, kwani sera ya Chadema ni kutokuwa na Rais wa Tanzania kutoka Zanzibar milele?” alihoji Fatma.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live