Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lipumba kushiriki maandamano kupinga mauaji Palestina

Picchaossupremeaslipumba Lipumba kushiriki maandamano kupinga mauaji Palestina

Fri, 5 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa chama cha Wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba Ijumaa April 05.2024 anatarajia kushiriki maandamano yaliyoandaliwa na waumini wa Kiislam wa dhehebu la Shia yanayolenga kupinga mauaji ya Halaiki na dhulma dhidi ya raia wa Palestina, yanayotarajiwa kufanyika Ilala Boma, Dar es Salaam

Taarifa ya chama hicho iliyotolewa leo, Alhamisi April 04.2024 na Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano kwa umma Taifa Mohamed Ngulangwa imeeleza kuwa Shia Duniani kote hutumia Ijumaa ya mwisho wa mwezi mtukufu wa Ramadhan kila mwaka kuadhimisha siku ya mshikamano na Wapalestina (QUDUS)

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, Prof. Lipumba atashiriki maandamano hayo kwa kuzingatia hali inayoendelea sasa nchini Palestina na kwa kuenzi msimamo wa kitaifa uliowekwa na waasisi wa Tanzania (Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Sheikh Abeid Amani Karume) ambao waliliachia Taifa heshima kubwa kwa kutetea wanyonge na kupinga dhulma kokote Duniani

Kuhusu mgogoro wa muda mrefu wa ukanda wa Gaza CUF imeeleza kuwa, msimamo wa Tanzania ulikuwa ni kusimama upande wa utetezi wa haki ya Wapalestina ambao kimsingi wanadaiwa kuteswa katika ardhi yao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live