Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lipumba atangaza mikutano ya hadhara, awavutia pumzi wabunge CUF

64580 Cuf+pic

Thu, 27 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Chama cha Wananchi (CUF) nchini Tanzania kimetangaza kuanza mikutano ya hadhara kuhamasisha watu kujitokeza kwenye shughuli ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.

Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amesema watafanya mikutano hiyo kwa kufuata taratibu huku akivitaka vyombo vya dola kutoingilia.

Mwenyekiti huyo ameyasema hayo leo Alhamisi Juni 27, 2019 wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Ofisi za CUF Buguruni jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuwasilisha maazimio ya Baraza Kuu la Uongozi la CUF lililokutana hivi karibuni.

Profesa Lipumba amevitaka vyombo hivyo kutoingilia uchaguzi wa serikali za mitaa na kuwaacha wananchi wapate haki yao ya kuchagua viongozi wanaowataka.

“Tutafanya mikutano kwa kuwa hilo si kosa kisheria tunaomba polisi na vyombo vingine vya dola wasituzuie,” amesema Profesa Lipumba

Amesema chama hicho kitafanya mikutano hiyo kwa nia njema ya kuisaidia Serikali ya Tanzania kuhamasisha watu wengi kujitokeza kujiandikisha.

Pia Soma

“Tume (ya uchaguzi -NEC) haina mvuto wa kuhamasisha watu, hiyo kazi inafanywa vyema na vyama vya siasa kwa kuongea na wananchi na kuwaeleza umuhimu wa kujiandikisha.”

“Hatuvunji sheria kwa kuwa hatutafanya kampeni mikutano yetu itakuwa ya amani na utulivu, tutakachotoa ni elimu na tutafanya kwa kufuata taratibu,” amesema Profesa Lipumba

Chanzo: mwananchi.co.tz