Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lipumba ajitabiria kutunukiwa tuzo ya MO Ibrahim akishinda Urais 2020

Profesa Ibrahim Lipumba AAAAAA 0 Lipumba ajitabiria kutunukiwa tuzo ya MO Ibrahim akishinda Urais 2020

Tue, 8 Sep 2020 Chanzo: millardayo.com

Chama cha wananchi CUF kimezindua rasmi kampeni zake katika viwanja vya Sabasaba mkoani Mtwara, ambapo mgombea wa Urais kupitia chama hicho Prof. Ibrahim Lipumba, amesema kama atachaguliwa atazingatia demokrasia na kuwa Rais wa kwanza atakayepata tuzo za MO Ibrahim.

Profesa Lipumba amesema kuwa tuzo hizo, hutolewa kwa Marais ambao wanazingatia demokrasia na kuheshimu haki za binadamu na kudai kuwa hilo litakuwa lengo lake.

”Mikoa ya kusini ina bahati ya kuwa na fukwe kubwa, Mgombea mwenza wangu ni mwekezaji katika Hoteli za kitalii amepita Lindi na Mtwara  anaiona Bahari, anaioina fursa ya kuweza kutumia kuwa na biashara kubwa za kitalii” Profesa Lipumba

”Kama kuna watu wana haki ya kuikataa CCM basi ni watu wa Kusini, mna Bahari lakini uvuvi unaofanyika ni uvuvi ulioduni na usio tumia vyombo vya kisasa, utastaajabu Tanzania tuna Bahari kubwa lakini eti tunavua Samaki wengi kwenye maji baridi kuliko baharini” Prof. Lipumba

MTOTO ALIEZIMIA KWA MIAKA 37 NA SIKU 111, HAKUZINDUKA AKAFA, MAMA ALIZIMIA MIAKA 27

Chanzo: millardayo.com