Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lipumba achokonoa dosari katika maridhiano

Lipumbaaapic Data Lipumba achokonoa dosari katika maridhiano

Fri, 15 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Pamoja na maelekezo mazuri ya Serikali kuhusu maridhiano, Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), Profesa Ibrahim Lipumba, amesema kumekosekana mipango thabiti ya kuyaweka katika mstari mzuri.

Hatua hiyo, amesema inachagiza kuibuka kwa changamoto katika utekelezaji wa maridhiano hayo.

Profesa Lipumba ameyasema hayo jijini Dar es Salaam leo, Septemba 15, 2023 alipohutubia hafla ya maadhimisho ya siku ya demokrasia nchini, iliyoandaliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).

"Maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu maridhiano ni mazuri, isipokuwa kuna changamoto katika kuyaweka katika mstari mzuri," amesema.

Kulingana na Profesa Lipumba ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, Rais Samia ana fursa muhimu ya kuandika historia kuhusiana na demokrasia nchini.

"Rais Samia anayo fursa ya kujiwekea historia ya kuweka misingi imara ya demokrasia, kutoka katika hali mbaya aliyoikuta," amesema.

Katika hatua nyingine, Profesa Lipumba amesema hivi karibuni ilifanyika mikutano kadhaa kuhusu demokrasia na mambo kadhaa wamekubaliana.

Miongoni mwa mambo hayo, Kiongozi huyo wa TCD amesema ni umuhimu wa kuwa na Katiba Mpya itakayoweka misingi mizuri ya demokrasia.

Lakini kutokana na muda mchache uliobaki kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Mkuu, Profesa Lipumba amesema wamekubaliana kuanza na mabadiliko madogo.

Mabadiliko hayo madogo kulingana na Mwenyekiti huyo wa TCD, yatahusisha kuweka mazingira mazuri ya kuwa na tume huru ya uchaguzi kabla ya uchaguzi wa 2024 na ule wa 2025.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live