Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lipumba: Lissu mvuruga demokrasia

912c55f6558da60bb49bfc13e31c7de0 Lipumba: Lissu mvuruga demokrasia

Sat, 29 Aug 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MGOMBEA wa urais wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amekishutumu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuwa kinakwamisha demokrasia.

Lipumba alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kitendo chamgombea wa urais kwa tiketi ya Chadema, Tundu Lissu kumwekea pingamizi wakati amefuata amefuata maelekezo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

“Sisi tunagombea ujenzi wa mfumo wa demokrasia watu wawe huru kusiwepo vizingiti. Lakini ni wazi kwamba Chadema hawana demokrasia wanakuwa wa kwamza kuweka vizingiti, ndiyo maana nasema wananiogopa,” alisema Profesa Lipumba.

Alisema anachoshangaa ni kwamba wanasiasa wote hususani wa vyama vya upinzani, wanachogombea ni ujenzi wa mfumo wa demokrasia ili watu wawe huru kusiwepo na vizingiti, lakini baadhi yao ndio wamekuwa wa kwanza kujitokeza kukwamisha juhudi hizo za demokrasia.

Lipumba alisema Chadema kinamuogopa kwenye siasa ndiyo maana kiliamua kumuwekea pingamizi lisilo na mashiko kufifisha nguvu yake.

“Lakini cha ajabu Lissu hakuwaona hao wengine akaamua kuniwekea mimi pingamizi ni wazi kwamba Chadema wananiogopa, wanajua hiki ni kigogo, kigogo cha mpingo hakitikisiki, na sidhani kama alizungumza na mwenzake kuhusu kuniwekea pingamizi hilo na mbaya zaidi pingamizi lenyewe halikuwa na hoja”,alisema Profesa Lipumba.

Aliongeza kuwa mbaya zaidi ni kwamba hata taarifa hizo Chadema walizipeleka kwenye mitandao ya kijamii hali iliyoleta taharuki miongoni mwa wanachama wa CUF kwamba mgombea wao hatagombea.

“Mbaya zaidi unaanza kupeleka kwenye mtandao wa kijamii lengo ni nini? kuleta vurugu kwa wanachama wapate mshutuko wasijue cha kufanya, sisi chama hatuna taarifa mnaweka mambo kwenye mtandao kuleta hofu na fujo ,wakati kuna mambo mazito kuyasema yenye hoja katika uchaguzi huu, lakini wewe(Lissu) unaleta hofu, ana ajenda gani? Lazima tujiulize,” alihoji.

Alisema hata vyama vya upinzani vilipoungana na kuunda Ukawa na kuandaa hoja nzito za kutaka mabadiliko ya demokrasia, hoja hizo zinaonekana wazi kwamba Chadema wanaweka vizingiti kusiwe na demokrasia.

Chanzo: habarileo.co.tz