Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lembeli alia kuanza kuchezewa rafu CCM

Lembeli Aibukia Mkutano Wa Magufuli Lembeli alia kuanza kuchezewa rafu CCM

Mon, 1 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

ALIYEKUWA Mbunge wa Jimbo la Kahama, James Lembeli, amesema anachukizwa na baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Kahama, wanaomtuhumu kwenye majukwaa ya kisiasa kuwa anafanya kampeni za chini chini kuwania Jimbo la Ushetu.

Lembeli alitoa malalamiko hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu namna viongozi wa CCM wanavyomtuhumu kwenye majukwaa kuwa anafanya harakati za kugombea nafasi hiyo.

Alisema hawezi kufanya kampeni za chini chini kuwania jimbo ambalo bado lina mbunge wake, lakini anashangazwa na maneno yanayosema na viongozi wa chama hicho wawapo majukwaani ndani ya jimbo kuwa anafanya kampeni na kulitaka jimbo.

Lembeli alisema pia anazushiwa kuwa alirejea katika chama hicho kutoka Chadema bila kufuata utaratibu.

Aidha, Lembeli alisema kugombea ni haki yake kisheria na kikatiba, na kwamba anaweza kugombea nafasi yoyote kwenye uchaguzi mkuu hata kama ni Jimbo la Arusha.

“Sitajatangaza kama nagombea, ila ukifika muda nitatangaza na kwenda kugombea nafasi gani na jimbo gani,” alisema.

Aidha, alisema aliondoka CCM kwa mambo kama hayo yanayoendelea kwa sasa, na kuongeza anafuata utaratibu uliowekwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa juu ya kutofanya kampeni kwenye jimbo ambalo lina mbunge na akikutana naye atamweleza yanayoendelea Kahama.

Kwa mujibu wa Lembeli, vyumba vya madarasa aliyoanzisha katika jimbo la Ushetu kwa kutumia fedha za mfuko wa jimbo, mpaka wakati huu hayajakamilishwa na badala yake wanaibuka na kujenga vyumba vipya vya madarasa shule za msingi na sekondari, na aliyoanzisha wanayaacha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live