Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lema awataka Monduli kutunza heshma ya Lowassa

16094 Pic+lema TanzaniaWeb

Fri, 7 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Monduli. Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema amewataka wakazi wa Monduli kumchagua mgombea ubunge kupitia Chadema ili kulinda hadhi na heshma ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni katika Kata ya Meserani, Lema alisema uchaguzi wa Monduli unafanyika baada ya aliyekuwa mbunge, Julius Kalanga kujiunga na CCM ili kummaliza nguvu Lowassa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa miaka 20.

“CCM wanataka kutumia uchaguzi huu kumdhoofisha Lowassa kuelekea uchaguzi wa 2020, hivyo wananchi wa Monduli msikubali Lowassa kudhoofishwa, huyu ni Laigwanani kiongozi wenu wa mila,” alisema

Kwa upande wake Lowassa, aliwataka wakazi wa Monduli kuwaaibisha CCM kwa kumchagua mgombea wa Chadema , Yonas Laizer kwani ana uwezo wa kuwasaidia.

Alisema CCM imepeleka Monduli wabunge 16 kupambana naye lakini wao wamchagua Laizer.

Chanzo: mwananchi.co.tz