Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lema aunga mkono kauli ya Rais Samia "Ndani ya Chadema kunawaka moto"

Lema Samia Lema aunga mkono kauli ya Rais Samia

Tue, 12 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa zamani wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema ameungana na kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyoitoa jana kwenye mkutano na vyama vya siasa kuwa ndani ya baadhi ya vyama vya siasa nchini kuna moto unawaka ndiyo maana hata wao wenyewe hawaelewani.

Lema ambaye chama chake cha CHADEMA hakikuhudhuria mkutano huo, amesema kuwa chama chao kimejengwa kwa misingi ya kuhoji na kupishana kwa hoja badala ya kukubali kila jambo, hivyo ni kweli kuna moto.

"Ninakubaliana na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kauli yake "Ndani yao kuna Moto" Chadema imejengwa ktk ujuzi wa kuhoji, kubishana, kupishana na hata kotofautiana wkt mwingine unaweza kuhisi watu wanapigana.

"Malezi ndani ya CDM hayajafanikiwa kukuza CHAWA. Hoja ndani ya vikao zina maana kubwa kuliko umri na nafasi.Mkti Mbowe amefanikiwa sana kujenga Chama chenye sura hii na ndio maana CHADEMA leo ni tumaini kubwa.

"CHADEMA ina uwezo wa kulea na hata kufukuza wasio na malengo ya dhati kwa Wananchi. Wengine walishindwa kuheshimu misingi ya kweli waligeukia kwenu na wakawa viongozi wakubwa huku wengine wakiitwa wapinzani kumbe ni wafuasi wa sera/nyimbo zenu.

"CHADEMA kuna moto sana kwa sababu CHAWA hawana mazingira mazuri ya kazi.CHADEMA inaamini kwamba Mindset Transformation ni hatua muhimu ktk maendeleo ya Nchi.

"CHADEMA siku zote kuna moto hata sasa kuna moto maana Taifa linapita katika wakati ngumu sana na gharama za maisha ya watu zinaendelea kuwa ngumu.CHADEMA lazima vichwa vyao vipate moto," amesema Lema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live