Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lema ampongeza CAG kwa ujasiri, kusimamia Katiba

Video Archive
Thu, 11 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Mbunge wa Arusha mjini (Chadema) Godbless Lema amempongeza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad kwa ujasiri wake na kuilinda na kutetea Katiba huku akitaka taarifa hiyo kufanyiwa kazi ipasavyo.

Akizungumza na Mwananchi leo kuhusiana na taarifa ya CAG ambayo imewasilishwa bungeni leo, Lema amesema kama CAG angekuwa mtu dhaifu angekuwa tayari amejiuzuru kutokana na maazimio ya Bunge.

"Duniani tuna watu wachache sana waadilifu na wenye uwezo kama Profesa Assad, taifa tunapaswa kujivunia na kumuunga mkono na siyo kumkatisha tamaa kutokana na kazi ambazo anafanya kwa maslahi ya taifa hili," amesema.

Lema amesema Profesa Assad amesimamia Katiba  na ameonesha hakuna ambaye yupo juu ya Katiba na kwamba ameweza kuendelea na kazi yake kwa uadilifu mkubwa kwa kutoa taarifa ambayo sasa inapaswa kufanyiwa kazi.

"Amesimamia Katiba, hoja na uadilifu, ametoa mapungufu mengi katika matumizi ya Serikali, vyama vya siasa na mashirika ya umma, ingawa  kuna mengine hayajawekwa wazi, lakini  uwezo wake  umejidhihirisha," amesema.

Akizungumzia yaliyogunduliwa na CAG, ikiwapo ununuzi wa gari la Chadema na CCM kutotoa makato ya wafanyakazi, alisema ana amini majibu yatatolewa na kwa upande wa Chadema alisema suala hilo litatolewa ufafanuzi na viongozi wa kitaifa kwani hakuna ubadhirifu.

Related Content

Lema amesimamishwa na bunge kuhudhuria mikutano mitatu ya bunge baada ya kutoa kauli bungeni kuwa bunge ni dhaifu akiunga mkono kauli ya CAG na mbunge wa Kawe, Halima Mdee.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz