Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lema, Zitto kimeuamana!

Lema Na Zitto.jpeg Lema na Zitto

Sun, 13 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Unaweza kusema ni Mvutano wa maneno kati ya Mbunge wa zamani wa Arusha Mjini Godbless Lema na Kiongozi wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe.

Kupitia mtandao wa Twitter Godbless Lema ameandika Ujumbe ambao unamuelezea kijana mmoja huku akimfananisha na Mwenyekiti wa TLP Agustino Mrema.

Lema ameandika "Kuna Kijana mmoja ana behave na anataka aonekane kama Mpinzani wa kweli huku kimsingi yeye ni kama Mrema wa TLP lakini yeye akiwa mchangamfu zaidi.."

Katika Ujumbe huo ambao hakutaja jina la kijana huyo, ulimuibua Kiongozi wa ACT Wazalendo na Mbunge wa zamani Zitto Kabwe.

Zitto amejibu kwa kusema; "Kijana huyo ndiye aliyekutoa Wewe kwa Mrema ukaingia ulipo sasa Mwaka 2007. Kijana huyo huyo kwa kushiriakiana na wadau wakiwemo viongozi wako wa sasa ndio wataweka mazingira mazuri ya siasa. Endelea wailing sisi tunakuwekea mazingira mazuri ya kufanya siasa..."

Huu ni muendelezo wa mvutano baina ya wabunge hawa wawili wa zamani kutoka upinzani ambao wamewahi kuwa chama kimoja cha CHADEMA.

Zitto ni Miongoni mwa viongozi wa Upinzani ambao wapo katika kamati maalumu iliyoundwa na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ya kupitia hoja zilizojitokeza katika mkutano wa wadau wa Siasa na vyama uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana, mkutano ambao Chadema hawakushiriki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live