Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lema: Prof. Jay amenituma kufanya mkutano Mikumi

Lema JayA0012 Lema: Prof. Jay amenituma kufanya mkutano Mikumi

Sun, 9 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Chadema, Kanda ya Kaskazini, Godbless Lema amesema ameombwa na aliyekuwa Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule (Profesa Jay) kufanya mkutano wa hadhara jimboni humo.

Lema ameyasema hayo leo Jumapili Julai 9, 2023 baada ya kwenda kumjulia hali na msanii huyo mkongwe Profesa Jay aliyeugua kwa muda mrefu.

“Mungu ni mwema sana, baada ya muda mrefu kukutana tena na rafiki yangu Prof Jay. Ukimsikiliza unagundua kuwa wauuguzi wanaweza kujaribu kutibu lakini mponyaji ni Mungu peke yake,”amesema.

“Kaniomba niende Mikumi kufanya mkutano wa hadhara hivi karibuni huku akijianda kuja. Mikumi ninakuja,” amemalizia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live