Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lema: Nimechoka lakini nagombea

67f48635c9f908cacec9771d9d3cc57e Lema: Nimechoka lakini nagombea

Mon, 20 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema (pichani) amesema mwili wake umechoka lakini nafsi yake inamsukuma aendelee kugombea ubunge jimboni humo.

Lema aliema kushinda kwake kwenye kura za maoni kunampa nguvu kupambana katika jimbo hilo ili aweze kupata kura nyingi awe Mbunge kwa mara ya tatu.

Aliyasema hayo juzi wakati akiwashukuru wajumbe wa mkutano wa Chadema waliompitisha katika kura za maoni. Kwa mujibu wa Lema, wakati akiwa Mbunge kwa vipindi viwili alikumbana na mambo mbalimbali zikiwemo kesi mahakamani, kwenda magereza na kutohudhuria vikao vya Bunge la Tanzania kwa sababu ya kuwatetea wananchi.

Alisema hivi sasa kuna hofu miongoni mwa wanachama kwa kuwa madiwani wamekihama chama lakini wasife moyo na kwamba kwani kamati Kuu ya chama hicho itachagua watakaofaa kugombea ubunge.

“Kuna hofu madiwani wamekimbia kwenye kura za maoni chama kitawaachia mchague ila kwenye intelejensia ya Chadema vitu tutaamua nani ni nani, hatuwezi kuchagua watu halafu baadaye wanapandisha mabega, “alisema.

Alisema, kama wangemnyima kura angekiacha cheo cha Mwenyekiti wa Chadema, Kanda ya Kaskazini.

Chanzo: habarileo.co.tz