Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lema: Kuna siku inakuja, ma-RC, ma-DC mtajuta sana!

Lema Mongella Lema: Kuna siku inakuja, mtajuta sana

Tue, 12 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyewahi kuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amewaonya wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya nchini kufanya kazi zao bila kuwaonea watu kwani vyeo walivyo navyo ipo siku vitaondoka na watabaki kuwa raia wa kawaida.

Lema amesema hayo akimweleza Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella kufuatia kukamatwa kwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu mkoani humo kwa tuhuma za uchochezi ambaye hata hivyo tayari ameshaachiwa kwa dhamana.

"Umeogopa kufukuzwa kazi kwa gharama ya kuwa mjinga? Angalia nyuma ya kiti chako ukutani hayo majina unayo yaona wote walikuwa wakuu wa Mkoa Arusha kabla yako wewe. Wengine walikuwepo wakati wa Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete.

"Kwa nini mnayapa maisha yenu thamani ndogo kwa sababu ya ukuu wa mkoa au wilaya? Kuna siku inakuja ambayo wote mliokuwa maofisini mtajuta sana, kwani mtagundua kuwa mlishiriki kuharibu future za watoto na wajukuu zenu.

"Nyumba mnazojenga hawataishi na mashamba mnayo nunua kwa ajili yao hawatalima wala kuvuna.Linda nafsi yako ukiona unafanya yasiyo haki na kimbilia madhabauni na tubu kwa machozi,hakuna ubaya wala wema usio na malipo.

"Mara nyingi huwa mnasema sisi tunapokea maelekezo na kweli yanaweza kuwa ni maelekezo, je, unaweza kuelekezwa kutembea uchi hadharani na ukafanya?

"Kiburi kinachopinga uovu kina heshima kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu na nafsi zetu. Huu ujumbe usomwe wenzako wote," amesema Lema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live