Tue, 3 Jan 2023
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi wa kitaifa wa vyama vya siasa nchini, Ikulu jijini Dar es Salaam leo tarehe 03 januari, 2023
Kikao hicho kinachofanyikiwa Ikulu jijini Dar es Salaam, kila chama kinawakilishwa na watu wanne, mwenyekiti, makamu wenyeviti wawili wa Bara na Zanzibar pamoja na katibu mkuu.
Miongoni mwa viongozi hao ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live