Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

LIPUMBA:NITAKUWA RAIS WAKWANZA KUPEWA TUNZO

Lipumba 3?fit=800%2C445 LIPUMBA:NITAKUWA RAIS WAKWANZA KUPEWA TUNZO

Tue, 8 Sep 2020 Chanzo: zanzibar24.co.tz

Mgombea wa Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha wanachi CUF Prof Ibrahim Lipumba, amesema kama atachaguliwa atazingatia demokrasia na kuwa Rais wa kwanza atakayepata tuzo za Mo Ibrahim.

Hayo ameyabainisha jana Septemba 7, 2020, wakati akizundua rasmi kampeni zake katika viwanja vya Sabasaba mkoani Mtwara na kusema hutolewa kwa Marais ambao wanazingatia demokrasia na kuheshimu haki za binadamu na kudai kuwa hilo litakuwa lengo lake.

”Mikoa ya kusini ina bahati ya kuwa na fukwe kubwa,Mgombea mwenza wangu ni mwekezaji katika wa Hoteli za kitalii amepita Lindi na Mtwara anaiona Bahari, anaioina fursa za kuweza kutumia kuwa na biashara kubwa za kitalii”, amesema Profesa Lipumba.

”Kama kuna watu wana haki ya kuikataa CCM basi ni watu wa Kusini,mna Bahari lakini uvuvi unaofanyika ni uvuvi ulioduni na usio tumia vyombo vya kisasa, utastaajabu Tanzania tuna Bahari kubwa lakini eti tunavua Samaki wengi kwenye maji baridi kuliko baharini”, ameongeza

Chanzo: zanzibar24.co.tz