Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

LHRC na banio kufumua mfumo wa uchaguzi

Kikosipiic Data LHRC na banio kufunmua mfumo wa uchaguzi

Thu, 24 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

aada ya kikosi kazi cha kuratibu maoni ya wadau wa demokrasia ya vyama vya siasa kukabidhi mapendekezo ikulu, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimetoa mapendekezo 17 kikitaka kufumuliwa kwa mfumo mzima wa uchaguzi nchini.

Juzi kikosi kazi kinachoongozwa na Profesa Rwekaza Mukandala kilipendeleza mambo manane, likiwemo la mchakato wa Katiba mpya kuanza baada ya uchaguzi mkuu wa 2025, kurekebisha tume ya uchaguzi na uchaguzi wa mitaa kutosimamiwa na Tamisemi.

Kufuatia mapendekezo hayo ambayo Rais Samia Suluhu Hasssan aliagiza yaendelee kufanyiwa kazi, LHRC ilitoa mapendekezo yake, yakiwemo matano ya jumla ambayo ni kuruhusu matokeo ya rais kupingwa mahakamani na kuweka mfumo wa 50+1 kuwa kigezo cha ushindi katika uchaguzi wa rais.

Mengini ni Jeshi la Polisi kutoingilia shughuli za vyama vya siasa, usawa jinsia katika uwakilishi na kuwepo wagombea binafsi katika ngazo zote za uchaguzi.

Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Anna Henga aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuwa mapendekezo hayo yanalenga kupunguza baadhi ya vikwazo ambavyo si vya lazima wakati wa uchaguzi.

Alitolea mfano mfumo wa 50+1 kama kigezo cha ushindi kwamba kitaongeza uwazi, uwajibikaji na kupunguza tuhuma za wizi wa kura zinazotolewa na baadhi ya wanasiasa.

Advertisement Alisema mbali na kupendekeza mfumo huo, pia LHRC ilipendekeza kuondolewa kigezo cha mgombea kupita bila kupingwa na kutaka mgombea binafsi aruhusiwe katika ngazi mbalimbali ili kupunguza urasimu wa vyama ambavyo hutumia sifa ya uanachama.

Aidha alisema pendekezo la kutaka Jeshi la Polisi kutoingilia shughuli za vyama vya siasa kabla, wakati na baada ya kampeni kinyume na sheria linalenga kuhakikisha mikutano inafanyika kwa usawa.

Vilevile, alishauri matokeo ya kiti cha urais yawe yanapingwa mahakamani ikiwa kutakuwa na malalamiko ya msingi, kama ilivyoamuliwa na mahakama ya Afrika ya Haki za binadamu.

Kwa upande wa masuala ya jinsia katika uongozi, LHRC imependekeza kuwa na uwakilishi sawa wa kijinsia wa 50/50 kwa kuweka kipengele mahususi kitakachoweka sharti kwa sera au sheria yoyote kuzingatia usawa wa kijinsia.

“Hata kwa upande wa sheria ya vyama vya siasa kuwe na takwa la kisheria kwa vyama vya siasa kuzingatia usawa wa kijinsia, na watu wenye ulemavu wakati wa mchakato wa uteuzi,” alisema.

Pia aligusia umuhimu wa kufanyika mabadiliko katika nafasi mbalimbali, ikiwemo nafasi ya msajili wa vyama vya siasa, kuwa iwe inatangazwa na kuombwa hadharani kwa kuzingatia vigezo vitakavyoainishwa na kamati maalumu ya kuajiri.

Vilevile, LHRC ilipendekeza kufanyika kwa mabadiliko ya sheria ya uchaguzi katika upatikanaji wa watumishi wa tume.

Alitolea mfano, wakurugenzi wa halmashauri zote nchini wasiwe wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya jimbo na wajikite katika majukumu ya kutumikia wananchi.

Pia alisema kwa upande wa mkurugenzi wa uchaguzi, mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi na makamishna wapatikane kwa kuomba kazi ambazo zitatangazwa ili kuondoa mgogoro wa kimasilahi kwa chama fulani.

Kuhusu mchakato wa Katiba kusogezwa hadi baada ya uchaguzi wa 2025, Henga alisema “mapendekezo hayo hata Rais Samia pia ameyakubali kwamba yafanyike mabadiliko madogo ya baadhi ya sheria, ikiwemo sheria za vyama ambazo zimekuwa zikilalamikiwa sana, hivyo hata ikiwa 2025 maadamu mchakato huo utafufuliwa, ni sawa.”

Katibu Mkuu wa ADC, Hassan Doyo ameungana na Henga kuwa mchakato wa Katiba mpya uanze baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, akisema suala hilo limekaa vema na litafanyika bila tatizo.

“Sasa hivi tumeshajua kuwa mwaka 2025 mchakato wa Katiba mpya utaanza, tofauti na mwanzo ambapo hatukujua hilo. Nakubaliana na hoja za kikosi kazi kuwa muda huo ni sahihi kwa ajili ya mchakato huo, wapo sahihi katika hilo,” alisema Doyo.

Hata Katibu Mkuu wa NRA, Hassan Almas alisema: “Kilichopendekezwa na kikosi kazi hatuna sababu ya kukihoji kwa sababu kina nia njema. Tutahoji ikifika mwaka 2025 sio sasa”.

Hakuna sababu

Wakati Henga, Doyo na Almas wakisema hayo, baadhi ya wadau waliozungumza na Mwananchi jana kwa nyakati tofauti, walisema hawaoni sababu za mchakato wa Katiba mpya kufanyika baada ya mwaka 2025 kwa sababu hauna uhusiano wowote na shughuli za kimaendeleo wala kiuchaguzi, bali unabeba mambo ya namna ya kuendesha nchi na kiutawala.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live