Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwa hili, furaha ya Chadema inaizidi ya CCM

Kwa hili, furaha ya Chadema inaizidi ya CCM

Wed, 6 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Wafuasi wa Chadema mitaani walipoteza hamu naye. Edo wa Chadema siyo yule wa CCM. Baada ya kukosa urais 2015 alifeli kila kitu. Ni dhahiri huko CCM pia mchezo hakuucheza yeye bali kulikuwa na akili kubwa nyuma yake. Mwili ulikuwa mtaa wa Ufipa akili ilibaki viunga vya Lumumba.

Hakuwa yule wa kuzunguka kwenye taasisi za dini na watu binafsi. Akituaminisha kuwa ni mwamba wa siasa nchi hii. Kumbe yeye alikuwa mbele nyuma yake kukiwa na akili kubwa za Rostam na kina Nchimbi zikiendesha ‘gemu’. Hao ndo waliobaki na injini ya mipango Lumumba. Chadema ilienda bodi tu.

Wapo wanaodai karudi ili ‘kurahisisha kumtoa jela mkwe wake’. Kama kweli atakuwa mbinafsi kwani ni zaidi ya miaka mitatu mkwewe yuko jela. Kama ana huruma na penzi la bintiye angefanya maamuzi haya miaka mitatu iliyopita. Kwanini leo. Tundu Lissu akiwa kaanza fujo zake? Kasoma mchezo 2020 hauziki tena.

Wakati JK akimsikiliza Msigwa, Nape, Sugu au January ili kwenda na muda. Edo anataka kusikilizwa yeye tu. Akiamini siasa za mtandao ambazo zilifanikiwa utawala wa Mkapa. Waliogoma kuhama naye walijua wanachofanya. Kurudi CCM, ni furaha kwa Chadema kuliko Humphrey Polepole na makada wenzake.

Sikia hii: Kuna mwanasiasa alienda kijiji kimoja kufanya kampeni za uchaguzi. Akaanza kujinadi kwa mbwembwe nyingi sana kama kawaida yao na kumalizia kwa kuwauliza matatizo yao. Wale wanakijiji wakamueleza kuwa tatizo kubwa pale kijijini kwao ni ukosefu wa madaktari.

Mgombea huyo akachukua simu na kuanza kuongea. Alipomaliza akawaambia “tatizo lenu litaisha mara moja mkinichagua.” Hapo hapo akawauliza kama wana tatizo lingine. Wakasema hakuna ‘netiweki’ kabisa katika kijiji chao tangu taifa lipate uhuru. Umeelewa nini? Usiamini sana maneno ya wanasiasa.



Chanzo: mwananchi.co.tz