Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kuzuia mikutano ya siasa hata ya ndani nguvu ya ccm au ya upinzani?

34491 Pic+mikutano Tanzania Web Photo

Wed, 2 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

June 23, 2016, Rais John Magufuli alipiga marufuku vyama kufanya baadhi ya shughuli za siasa, hasa mikutano ya hadhara na maandamano mpaka 2020, ili ‘kutoa muda wa kutekeleza yale aliyoyaahidi kwa wanachi.’

Aliagiza wabunge na madiwani kufanya siasa katika majimbo yao tu, jambo lililoathiri viongozi wakuu wa upinzani katika harakati za ujenzi wa vyama kama sheria ya vyama vya siasa inavyotaka.  

Tangu kutangazwa kwa zuio hilo, viongozi wa vyama vya upinzani walikuwa wakipishana katika vituo vya polisi na mahakiama kutokana na kukaidi agizo hilo. Waathirika zaidi walionekana kutoka Chadema kwa kuwa ndio chama chenye shughuli nyingi. 

Kimyakimya agizo hilo limegusa hadi mikutano ya ndani. Agosti 2016, viongozi wakuu wa Chademawalikamatwa na polisi kwa mahojiano, wakati wakifanya kikao cha ndani kilichokuwa kikifanyika katika hoteli ya Giraffe, jijini Dar es salaam.  

Licha ya polisi kueleza mara kwa mara kuwa mikutano ya ndani si tatizo, bado limeendelea kutumia nguvu kuidhibiti, kuwakamata wahusika na mara nyingi kuachiwa kimya kimya bila wahusika kufikishwa mahakamani.

Kwa mfano, Desemba 16, mwaka jana,mkoani Iringa, Jeshi la Polisi lilimkamata Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho upande wa Zanzibar, Salum Mwalimu eneo la Mafinga akiwa anajiandaa kushiriki kikao cha ndani.  

Siku chache baadaye ,Jeshi hilo wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro lilizuia pia mkutano wa ndani na kisha kuwakamata Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Vincent Mashinji pamoja na viongozi wengine watatu kwa madai ya kufanya “mikusanyiko isiyokuwa halali kisheria”.

Hali nhiyo inaelezwa na wachambuzi wa siasa kuwa ni kujaribu kutumia nguvuza dola kuzioa nguvu za ya upinzani, hasa Chadema, baada ya kuonekana tishio mwaka 2015.

Profesa Gaudence Mpangalla wa Chuo Kikuu cha Ruaha mkoani Iringa anasema changamoto inazokabiliana nazo Chadema zinatokana na kuonekana tishio kisiasa katika uchaguzi wa mwaka 2015.

 “Harassment (manyanyaso) hii imelengwa zaidi kwa Chadema  kwa sababu wakiiachia sana inaweza kuwa tishio kwa uchaguzi ujao. Ni chama kilichoonyesha nguvu ya kutaka kuishinda CCM uchaguzi uliopita, ndiyo maana kimeandamwa sana kuliko vyama vingine, hiyo iko wazi kabisa,” anasema Profesa huyo wa siasa na Utawala bora.

Anasema ilikuwa ni lazima kwa chama chochote kilichopo madarakani kuhakikisha kinapambana na Chadema ili kudhoofisha nguvu yake na kupunguza kasi yake kuelekea mwaka 2020.

Lakini Profesa Mpangalla anasema bahati mbaya, nguvu inayotumika kudhoofisha nguvu ya chama hicho inaweza kuwa msaada kwake.

“Wakati mwingine unaweza kudhani mbinu unayotumia itakidhoofisha chama kumbe ndiyo unakipatia nguvu zaidi, kwa sababu wananchi wanaona kwamba chama hiki kinaonewa, viongozi wake wanafungwa, kwa hiyo wananchi wanapata political Sympathy (huruma) kwa hivyo ni bora ukaruhusu waendelee kuliko kuzuia,” anasema.

Si huyo tu, hata Mhadhiri kutoka Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala Bora, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Richard Mbunda anasema zuio la mikutano ya siasa ilikuwa ni wazo la kudhoofisha nguvu ya upinzani nchini kupitia mikutano ya hadhara na ya ndani.

Hata hivyo, Profesa Mbunda anasema mazingira ndiyo yanatabiri hali ya kisiasa kwa wakati husika huku akisisitiza umuhimu wa vyama vya siasa kupata nafasi ya kukutana na wananchi ili kuuza sera zao.

Suluhisho la hayo yote, linaelezwa na Wakili na mchambu wa masuala ya kisiasa nchini, Dk Onesmo Kyauke anayesema kuwabchama hicho na upinzani kwa ujumla kinatakiwa kutumia muhimili wa mahakama kutafuta tafsiri ya kisheria kuhusu ushiriki wa siasa kupiatiab mikutano ya ndani na ya hadhara.

Wakili huyo anasema hatua hiyo itatoa mwongozo utakaosaidia kutumika wakati wote katika ushiriki wa siasa.

Hali halisi

Siku za karibuni kumekuwa na kamatakamata ya viongozi wa Chadema kwenye mikutano ya ndani katika mikoa mbalimbali wakati katika ziara ya kichama, hali inayoelezwa na polisi kuwa inachagizwa na mazingira ya mikutano yao.

Endapo Chama hakitatoa taarifa ya mkutano wake kwa Polisi, Kamanda Issah anasema ni mazingira ya sasa yanawalazimu kutoa taarifa ili kulinda usalama wao

“Kwa hali ilivyo tete sasa hivi , watu wanavyozusha mambo, mara wanasema watu wasiojulikana, ni vizuri vyombo vyao vya usalama vikawaangalia, hatutawafuata kwenye mikutano yao lakini ni vizuri wakapita tu wakasema mtuangalie tuko sehemu Fulani, tujue mkutano angalau tuwe na ABC ya kuwaangalia,  cha msingi ni maridhiano tu,”anasema



Chanzo: mwananchi.co.tz