Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Kuna Wabunge wastaafu maisha yao magumu" Ndugai

115699032 9f4e022c E6e8 46aa 90f2 9fe91ea34eae.jpeg "Kuna Wabunge wastaafu maisha yao magumu" Ndugai

Sat, 26 Jun 2021 Chanzo: millardayo.com

Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema hakuna mtu yeyote anayelidai Bunge akisisitiza kuwa orodha ya madai iliyosambaa mitandaoni ni ya mwaka 2018.

Ameeleza hayo bungeni mjini Dodoma kuhusu suala hilo aliloliita kuwa ni upotoshaji unaolenga kulivuruga Bunge.

Kwa mujibu wa Ndugai kuna orodha ya majina inayozunguka kwenye mitandao ya kijamii ikidai kuna watu wanalidai Bunge  na baadhi ya majina yaliyomo kwenye orodha hiyo ni la mbunge wa zamani wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.

Kiongozi huyo amesema tangu kutolewa kwa tangazo hilo kwenye mitandao ya kijamii, simu yake imejaa jumbe wa waliokuwa wabunge katika Bunge la 11 wakimuleleza kuwa wanamdai.

“Kuna watu walipomaliza ubunge maisha yao ni magumu kweli, sasa anasikia kuwa anadai yaani ni tabu tupu, acheni, acheni jamani siyo kweli,”  Ndugai.

Spika amesema wabunge wote walilipwa stahiki zao akiwemo aliyepo ng’ambo ambaye hakumtaja jina ambaye alidai kuwa alipoingiziwa fedha benki zilichukuliwa zote kwa sababu alikuwa anadaiwa.

EXCLUSIVE: BILIONEA WA MPUNGA, MKULIMA ALIEITWA NA BILL GATE, GARI ZA KIFAHARI, JUMBA KIWANDA

Chanzo: millardayo.com