Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kuchauka apendekezwa kuwania ubunge Liwawe

13997 Pic+kachauka TanzaniaWeb

Mon, 27 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Liwale. Kamati ya Siasa ya CCM Wilaya ya Liwale mkoani Lindi, imempendekeza Zuberi Kuchauka apitishwe na chama hicho kuwa mgombea ubunge wa Liwale.

Kuchauka alikuwa mbunge wa Liwale kupitia CUF kabla ya kujiuzulu ubunge na kuhamia CCM Agosti 13, 2018 mbele ya mkutano wa waandishi wa habari wa katibu mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM Wilaya ya Liwale waliokutana leo Agosti 29, 2018 umeridhia kumpitisha Kuchauka.

  Kamati ya Siasa CCM Wilaya imependekeza jina la mgombea ubunge Zuberi Kuchauka na diwani Mustafa Mtegite awanie Kibutuka kupita bila kupingwa,

Mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo, Mohamed Kitura akizungumza na wajumbhe wa mkutano huo amesema baada ya mkutano huo kumpitisha, watapeleka jina lake ngazi ya juu kwa ajili ya kupitishwa.

Kwa maana hiyo, jina la Kuchauka litapelekwa kujadiliwa katika kikao cha Kamati Kuu ya CCM chenye mamlaka ya kuteua wagombea ubunge.

Kuchauka alisema hana maneno ya kusema ambayo yatafanana na heshima aliyopewa na CCM kuridhia kujiunga na chama na kupewa mjumbe wa halmashauri kuu kumsindikiza hadi jimboni.

Awali, katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa CCM, Kanali Ngemela Lubinga amesema lengo la safari yake ni kumsindikiza Kuchauka jimboni humo.

Lubinga amesema Kuchauka amejiunga na CCM baada ya kuona kazi nzuri inayofanywa na Rais John Magufuli ya kuwaletea maendeleo wananchi.

Chanzo: mwananchi.co.tz