Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kubenea kujenga kidato cha 5

09a4ec926edb556446572548b85622c6 Kubenea kujenga kidato cha 5

Fri, 16 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MGOMBEA ubunge katika jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya ACT-Wazalendo, Saed Kubenea amewaahidi wakazi wa jimbo hilo kuwajengea shule ya kidato cha tano na sita.

Aidha, ameahidi kuimarisha vyama vya michezo pamoja na kuondoa kodi ndogo kwa wafanyabiashara. Kubenea aliyasema hayo jana jimboni humo katika kata ya Mzimuni wakati akifanya kampeni ya mtaa kwa mtaa.

Alisema jimbo hilo halina shule za kidato cha tano na sita, hivyo atajenga shule hiyo ili watoto wa jimbo hilo wapate fursa ya kusoma kwenye shule hizo.

“Katika afya tunataka kuwa na vituo vya afya na kuimarisha hospitali za umma na kuhakikisha dawa zinapatikana na mtu aliyetimiza miaka 60 anapata huduma za tiba bure,”alisema.

Mgombea huyo pia alieleza kuwa ataimarisha vikundi vya vijana na kuwapatia mikopo ikiwemo kuanzisha kiwanda cha mbolea kinachotokana na taka ngumu.

“Fedha zipo kutoka Ujerumani na eneo lipo Mabwepande kinachokosekana ni mipango mizuri, sasa nikirudi Kinondoni nitaanzisha kiwanda cha mbolea ili kwenye masoko wasitozwe ushuru wa taka kwani sasa zitakuwa dili,” alisema mgombea huyo.

Pamoja na hayo alieleza sera yake katika upande wa michezo kuwa ni kuanzisha chombo cha kusimamia michezo kitakachoundwa kwa mujibu wa sheria ya bunge ambacho viongozi wake watapatikana kwa uadilifu wakiwa wasafi bila ushabiki wa vilabu mikubwa.

Mgombea mwenza wa urais kupitia CHADEMA, Salum Mwalimu akihutubia wananchi wa Kijiji cha Ulumi katika Jimbo la Kalambo mkoani Rukwa juzi wakati wa mkutano wa kampeni za uchaguzi mkuu uliofanyika kijijini hapo juzi.

Chanzo: habarileo.co.tz