Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kivuko champa wasiwasi Dk Tizeba ubunge 2020

Kivuko champa wasiwasi Dk Tizeba ubunge 2020

Fri, 1 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Waziri wa zamani wa Kilimo, Dk Charles Tizeba amesema ana wasiwasi  kuwa hatochaguliwa kuwa mbunge wa Buchosa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 kwa maelezo kuwa anahujumiwa.

Akizungumza leo Jumatano Oktoba 30, 2019 katika kikao cha kwanza cha mwaka wa fedha 2019/20 cha bodi ya barabara jijini Mwanza, mbunge huyo amesema Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa) wana mpango wa kumhujumu ashindwe ubunge.

Madai hayo yametokana na Temesa kuweka vivuko viwili halmashauri ya Buchosa yenye visiwa 28, wananchi kudai mbunge wao hafanyi kazi ipasavyo.

Tizeba akitoa mfano wa kisiwa cha Nkome kinachopatikana na Buchosa, kwamba kina wakazi zaidi ya 100,000 lakini kina kivuko chenye uwezo wa kubeba tani 50,  na tume zimeenda mara kadhaa lakini taarifa ya mhandisi wa Temesa inaonesha kivuko hicho kinafanya kazi nzuri kitu ambacho si kweli.

Meneja wa Temesa Mkoa wa Mwanza,  Karouda Hussein amekiri kuwepo hitaji la kivuko kingine  na kuwa walitaka kupeleka kivuko cha Mv Sabasaba lakini walishindwa kwa sababu walikipeleka kisiwa cha Ukara baada ya ajali ya kivuko cha Mv Nyerere mwaka, 2018.

Chanzo: mwananchi.co.tz