Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kitu ameongea Mbunge Ridhiwani kuhusu mahojiano ya Rais Samia

CHALINZE Ridhiwani Kikwete, Mbunge wa Chalinze

Tue, 10 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kufuatia mahojiano aliyofanya Rais Samia jana, kumeibuka na mijadala mingi katika mitandao ya kijamii kufuatia baadhi ya mambo aliyoyazungumzia hasa suala la kukamatwa kwa kiongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Freeman Aikael Mbowe, ambaye anatuhumiwa kwa makosa ya Ugaidi, suala la Tozo za miamala, suala la Uhuru wa kisiasa.

Baadhi ya wanasiasa wameibuka na mitazamo mingi huku kila mmoja akionesha namna ambavyo amepokea jumbe hizo.Ridhiwani Kikwete, Mbhunge wa Chalinze ni miongoni mwa waliotoa maoni yao kuhusu mahojiano hayo, huku akionesha kufurahishwa na muelekeo wa siasa za Rais Samia.

"nimeangalia Interview ya Rais Samia ni wazi kuwa amejitambulisha ni kiongozi mkweli, anayeheshimu taratibu, anaye tambua mapito ya nchi na anayejua tunachokitaka kwa manufaa ya wengi"

Mahojiano hayo hadi sasa bado ni gumzo kwa wananchi huku wakionesha mitazamo tofauti tofauti ya mapokeo yao kuhusu mambo yaliyojadiliwa katika kipindi hicho cha mahojiano

Chanzo: www.tanzaniaweb.live