Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kingu aipiga tafu UVCCM Ikungi

Kingu1 Kingu aipiga tafu UVCCM Ikungi

Mon, 18 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MBUNGE wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu ametoa mifuko 50 ya saruji yenye thamani ya shilingi 800,000 ili kusaidia kuanza kwa ujenzi wa nyumba ya Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Ikungi.

Kingu amekabidhi msaada huo jana kama sehemu ya kuunga mkono juhudi za umoja huo wa kujenga nyumba za makatibu wake ambapo siku chache zilizopita alitoa msaada wa mabati 60 yenye thamani ya shilingi 1,300,000 kwa ajili ya upauaji wa nyumba ya Katibu wa UVCCM mkoani humo.

“Kutokana na imani niliyo nayo kwa chama changu na UVCCM nimeona ni vyema kuunga mkono katika ujenzi huu kwa kununua mifuko hii 50 ya saruji ya kuanzia na kama mtaonesha moyo wa kujitoa nitahakikisha ujenzi wa nyumba hiyo unakamilika ndani ya wiki mbili” amesema Kingu.

Akipokea msaada huo kwa niaba ya kamati ya utekelezaji ya UVCCM Wilaya ya Ikungi, Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya, Jafari Dude, amemshukuru Mbunge huyo kwa msaada huo na moyo wa kujitoa katika shughuli mbalimbali za chama.

Mbali na msaada huo wa saruji pia Kingu ametoa viti 20 katika Kanisa la FPCT la Kijiji cha Nkuninkana wilayani humo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live